Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kumbukumbu la Torati 8:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mtakula na kushiba, mtamshukuru Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa nchi nzuri aliyowapa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mtakula na kushiba, mtamshukuru Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa nchi nzuri aliyowapa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mtakula na kushiba, mtamshukuru Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa nchi nzuri aliyowapa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mtakapokwisha kula na kushiba, msifuni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa ajili ya nchi nzuri aliyowapa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wakati mtakapokwisha kula na kushiba, msifuni bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa ajili ya nchi nzuri aliyowapa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kumbukumbu la Torati 8:10
14 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.


Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote.


Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.


Na nimwimbie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu kuhusu shamba lake la mizabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu, Kilimani penye kuzaa sana;


Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.


Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano.


(lakini zikaja mashua nyingine kutoka Tiberia mpaka karibu na mahali pale walipokula mikate, wakati Bwana aliposhukuru.)


Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.


Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.


Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu.


nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake mnaweza kuchimba shamba.


shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.