Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Kumbukumbu la Torati 8:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Amri hii ninayokuamuru leo mtaizingatia, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo BWANA aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Amri zote ninazowapeni leo, lazima mzifuate kwa uangalifu ili mpate kuishi na kuongezeka, mpate kuingia na kuimiliki ile nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliapa kuwapa babu zenu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Amri zote ninazowapeni leo, lazima mzifuate kwa uangalifu ili mpate kuishi na kuongezeka, mpate kuingia na kuimiliki ile nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliapa kuwapa babu zenu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Amri zote ninazowapeni leo, lazima mzifuate kwa uangalifu ili mpate kuishi na kuongezeka, mpate kuingia na kuimiliki ile nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliapa kuwapa babu zenu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Uwe mwangalifu kufuata kila agizo ninalokupa wewe leo, ili mweze kuishi, kuongezeka na mweze kuingia mkamiliki nchi ambayo Mwenyezi Mungu aliahidi kwa kiapo kwa baba zenu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Uwe mwangalifu kufuata kila agizo ninalokupa wewe leo, ili mweze kuishi, kuongezeka na mweze kuingia mkamiliki nchi ambayo bwana aliahidi kwa kiapo kwa baba zenu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Amri hii ninayokuamuru leo mtaizingatia, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo BWANA aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Kumbukumbu la Torati 8:1
9 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi ni BWANA, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda;

Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.

Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.

Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na BWANA, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kulia wala wa kushoto.

Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.

Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.