Kumbukumbu la Torati 6:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tena itakuwa haki kwetu, tukizingatia kufanya maagizo haya yote mbele ya BWANA, Mungu wetu, kama alivyotuagiza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena tutakuwa waadilifu kama tukitimiza kwa uangalifu amri hizi zote mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama alivyotuamuru’. Biblia Habari Njema - BHND Tena tutakuwa waadilifu kama tukitimiza kwa uangalifu amri hizi zote mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama alivyotuamuru’. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena tutakuwa waadilifu kama tukitimiza kwa uangalifu amri hizi zote mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama alivyotuamuru’. Neno: Bibilia Takatifu Tukizitii kwa bidii amri hizi zote mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kama alivyotuamuru sisi, hiyo itakuwa haki yetu.” Neno: Maandiko Matakatifu Kama tukizitii kwa bidii amri hizi zote mbele za bwana Mwenyezi Mungu wetu, kama alivyotuamuru sisi, hiyo itakuwa haki yetu.” BIBLIA KISWAHILI Tena itakuwa haki kwetu, tukizingatia kufanya maagizo haya yote mbele za BWANA, Mungu wetu, kama alivyotuagiza. |
Wamwekee Mungu tumaini lao. Wala wasiyasahau matendo ya Mungu, Bali wazishike amri zake.
tena ikiwa amezifuata sheria zangu, na kuzishika hukumu zangu; mtu huyu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema Bwana MUNGU.
Nikawapa amri zangu, na kuwaonesha hukumu zangu, ambazo mwanadamu ataishi kwazo, kama akizitenda.
Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na maagizo yangu yeyote atakayefanya hivyo ataishi; mimi ndimi BWANA.
Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.
Sharti umrudishie rehani lichwapo jua, apate kulala na mavazi yake, na kukubarikia; nayo itakuwa ni haki kwako mbele za BWANA, Mungu wako.
Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.