hao ambao BWANA alifanya agano nao, akawaamuru, akasema, Msiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuitumikia, wala kuitolea sadaka;
Kumbukumbu la Torati 6:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msiabudu miungu mingine, miungu ya watu walio jirani nanyi, Biblia Habari Njema - BHND Msiabudu miungu mingine, miungu ya watu walio jirani nanyi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msiabudu miungu mingine, miungu ya watu walio jirani nanyi, Neno: Bibilia Takatifu Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka; Neno: Maandiko Matakatifu Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka; BIBLIA KISWAHILI Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao; |
hao ambao BWANA alifanya agano nao, akawaamuru, akasema, Msiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuitumikia, wala kuitolea sadaka;
wala msiwafuate miungu mingine, ili kuwatumikia na kuwasujudia, wala msinikasirishe kwa kazi ya mikono yenu; basi, mimi sitawadhuru ninyi kwa dhara lolote.
Pia niliwatuma watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiwatuma pasipo kukoma, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiifuate miungu mingine, ili kuitumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza.
kama hamwonei mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, wala kuifuata miungu mingine kwa hasara yenu wenyewe;
na laana ni hapo msipotii maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkapotoka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
katika miungu ya mataifa yaliyo kandokando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia;
Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawaonya leo ya kuwa mtaangamia bila shaka.
Msiingie kati ya mataifa haya, yaani, haya yaliyobaki kati yenu; wala msitaje majina ya miungu yao, wala kuwaapisha watu kwa majina hayo, wala kuitumikia, wala kujiinamisha mbele yao;