Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Kumbukumbu la Torati 5:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nenda karibu wewe, ukasikie yote atakayoyasema BWANA, Mungu wetu; ukatuambie yote atakayokuambia BWANA, Mungu wetu; nasi tutayasikia na kuyatenda.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Heri wewe Mose uende karibu, ukasikilize yote atakayosema Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kisha uje kutuambia mambo hayo yote atakayokuambia. Sisi tutayasikiliza na kuyatekeleza’.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Heri wewe Mose uende karibu, ukasikilize yote atakayosema Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kisha uje kutuambia mambo hayo yote atakayokuambia. Sisi tutayasikiliza na kuyatekeleza’.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Heri wewe Mose uende karibu, ukasikilize yote atakayosema Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kisha uje kutuambia mambo hayo yote atakayokuambia. Sisi tutayasikiliza na kuyatekeleza’.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Sogea karibu usikie yale yote asemayo Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Sogea karibu usikie yale yote asemayo bwana Mwenyezi Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho bwana Mwenyezi Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nenda karibu wewe, ukasikie yote atakayoyasema BWANA, Mungu wetu; ukatuambie yote atakayokuambia BWANA, Mungu wetu; nasi tutayasikia na kuyatenda.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Kumbukumbu la Torati 5:27
11 Marejeleo ya Msalaba  

nawe utawafundisha zile amri na sheria, nawe utawaonesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo inawapasa kuifanya.

Watu wote wakaitika pamoja wakisema, Hayo yote aliyoyasema BWANA tutayatenda. Naye Musa akamwambia BWANA maneno ya hao watu.

Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali.

Wakamwambia Musa, Sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa.

Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya BWANA, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena BWANA tutayatenda.

Wakamwambia Yeremia, BWANA na awe shahidi wa kweli na uaminifu kati yetu; ikiwa hatufanyi sawasawa na neno lile, ambalo BWANA, Mungu wako, atakutuma utuletee.

Likiwa jema, au likiwa baya, sisi tutaitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake; ipate kuwa faida yetu, tunapoitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.

Maana katika watu wote ni nani aliyeisikia sauti ya Mungu aliye hai, akisema toka kati ya moto, kama vile sisi, asife?

Naye BWANA akasikia sauti ya maneno yenu mliyoniambia; BWANA akaniambia, Nimesikia sauti ya maneno ya watu hawa waliyokuambia; wamesema vema yote waliyosema.

na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lolote lingine;

Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, BWANA, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii.