Yakobo akapaita mahali pale, Penieli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.
Kumbukumbu la Torati 5:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC mkasema, Tazama, BWANA, Mungu wetu, ametuonesha utukufu wake, na ukuu wake, nasi tunasikia sauti yake toka kati ya moto; mmeona leo ya kuwa Mungu husema na mwanadamu, naye akaishi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema wakasema, ‘Sikiliza! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametufunulia utukufu na ukuu wake; tumeisikia sauti yake kutoka katikati ya ule moto. Leo hivi tumemwona Mungu akiongea na binadamu, naye binadamu badala ya kufa akaendelea kuishi! Biblia Habari Njema - BHND wakasema, ‘Sikiliza! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametufunulia utukufu na ukuu wake; tumeisikia sauti yake kutoka katikati ya ule moto. Leo hivi tumemwona Mungu akiongea na binadamu, naye binadamu badala ya kufa akaendelea kuishi! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza wakasema, ‘Sikiliza! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametufunulia utukufu na ukuu wake; tumeisikia sauti yake kutoka katikati ya ule moto. Leo hivi tumemwona Mungu akiongea na binadamu, naye binadamu badala ya kufa akaendelea kuishi! Neno: Bibilia Takatifu Nanyi mkasema, “Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ametuonesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kati ya moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye. Neno: Maandiko Matakatifu Nanyi mkasema, “bwana Mwenyezi Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye. BIBLIA KISWAHILI mkasema, Tazama, BWANA, Mungu wetu, ametuonesha utukufu wake, na ukuu wake, nasi tunasikia sauti yake toka kati ya moto; mmeona leo ya kuwa Mungu husema na mwanadamu, naye akaishi. |
Yakobo akapaita mahali pale, Penieli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.
Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti.
BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni.
kisha watawaambia wenyeji wa nchi hii; wamesikia wao ya kuwa wewe BWANA u kati ya watu hawa; maana, wewe BWANA waonekana uso kwa uso, na wingu lako lasimama juu yao, kisha wewe watangulia mbele yao, katika nguzo ya wingu mchana, na katika nguzo ya moto usiku.
Je! Kuna wakati wowote watu wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, na wakaendelea kuishi?
Ikawa, mlipoisikia sauti ile toka kati ya giza, na wakati uo huo mlima ule ulikuwa ukiwaka moto, basi, mlinikaribia, naam, wakuu wote wa makabila yenu, na wazee wenu,
Sasa basi, mbona tufe? Maana moto huu mkubwa utatuteketeza; tukiisikia tena sauti ya BWANA, Mungu wetu, tutakufa.