Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba, na kuingia katika bahari; maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yatakuwa safi.
Kumbukumbu la Torati 4:49 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na Araba yote iliyo ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, hata mpaka bahari ya Araba, chini ya materemko ya Pisga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema pamoja na eneo lote mashariki ya mto Yordani mpaka bahari ya Araba, mwishoni mwa miteremko ya mlima Pisga. Biblia Habari Njema - BHND pamoja na eneo lote mashariki ya mto Yordani mpaka bahari ya Araba, mwishoni mwa miteremko ya mlima Pisga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza pamoja na eneo lote mashariki ya mto Yordani mpaka bahari ya Araba, mwishoni mwa miteremko ya mlima Pisga. Neno: Bibilia Takatifu pamoja na eneo lote la Araba mashariki mwa Yordani, na kuenea hadi Bahari ya Araba kwenye miteremko ya Pisga. Neno: Maandiko Matakatifu pamoja na eneo lote la Araba mashariki ya Yordani, na kuenea mpaka Bahari ya Araba kwenye miteremko ya Pisga. BIBLIA KISWAHILI na Araba yote iliyo ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, mpaka bahari ya Araba, chini ya materemko ya Pisga. |
Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba, na kuingia katika bahari; maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yatakuwa safi.
na nchi ya Araba nayo, na mto wa Yordani, na mpaka wake, tokea Kinerethi mpaka bahari ya hiyo Araba, nayo ni Bahari ya Chumvi, chini ya materemko ya Pisga, upande wa mashariki.
Musa akapanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo, hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko. BWANA akamwonesha nchi yote ya Gileadi hata Dani;
toka Aroeri, iliyo juu ya ukingoni pa bonde la Arnoni, hadi mlima wa Sioni (nao ndio Hermoni),
Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu nisemazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuzizingatia.