uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;
Kumbukumbu la Torati 4:45 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC haya ndiyo maagizo, amri na hukumu, Musa alizowaambia wana wa Israeli walipotoka Misri; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Haya ndiyo maamuzi, masharti na maagizo ambayo Mose aliwaambia Waisraeli walipotoka Misri, Biblia Habari Njema - BHND Haya ndiyo maamuzi, masharti na maagizo ambayo Mose aliwaambia Waisraeli walipotoka Misri, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Haya ndiyo maamuzi, masharti na maagizo ambayo Mose aliwaambia Waisraeli walipotoka Misri, Neno: Bibilia Takatifu Haya ndio masharti, amri na sheria Musa alizowapa Waisraeli walipotoka Misri, Neno: Maandiko Matakatifu Haya ndiyo masharti, amri na sheria Musa aliyowapa wana wa Israeli wakati walitoka Misri, BIBLIA KISWAHILI haya ndiyo maagizo, amri na hukumu, Musa alizowaambia wana wa Israeli walipotoka Misri; |
uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;
Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.
ng'ambo ya Yordani, katika bonde lililoelekea Beth-peori, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni ndiye aliyepigwa na Musa na wana wa Israeli, walipotoka Misri;
Zishikeni kwa bidii sheria za BWANA, Mungu wenu, na maagizo yake, na amri zake alizokuagiza.
Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, Ni nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu?