na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.
Kumbukumbu la Torati 4:44 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na torati Musa aliyowawekea wana wa Israeli ni hii; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hii ndiyo sheria ambayo Mose aliwapa Waisraeli. Biblia Habari Njema - BHND Hii ndiyo sheria ambayo Mose aliwapa Waisraeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hii ndiyo sheria ambayo Mose aliwapa Waisraeli. Neno: Bibilia Takatifu Hii ndiyo sheria Musa aliyoweka mbele ya Waisraeli. Neno: Maandiko Matakatifu Hii ndiyo sheria Musa aliyoweka mbele ya Waisraeli. BIBLIA KISWAHILI Na torati Musa aliyowawekea wana wa Israeli ni hii; |
na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.
Haya ndiyo maagizo, BWANA aliyomwagiza Musa kwa ajili ya wana wa Israeli katika mlima wa Sinai.
Ikumbukeni Torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.
Haya ndiyo maagizo na hukumu, ambayo BWANA aliwaagiza wana wa Israeli, kwa mkono wa Musa, hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.
Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.
uyaandike maneno yote ya torati hii juu yake, utakapokwisha kuvuka; ili upate kuingia nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nchi imiminikayo maziwa na asali, kama alivyokuahidi BWANA, Mungu wa baba zako.
nayo ni hii, Beseri ya barani iliyo katika nchi tambarare, kwa Wareubeni; na Ramothi iliyo Gileadi, kwa Wagadi; na Golani iliyo Bashani, kwa Wamanase.
Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng'ambo ya pili ya Yordani, upande wa maawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki;