Na hiyo miji mtakayowapa Walawi, itakuwa miji sita ya kukimbilia, mtakayoweka kwa ajili ya mwenye kumwua mtu, ili akimbilie huko; pamoja na hiyo mtawapa miji arubaini na miwili zaidi.
Kumbukumbu la Torati 4:41 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo Musa akabagua miji mitatu ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndipo Mose akatenga miji mitatu mashariki ya mto Yordani, Biblia Habari Njema - BHND Ndipo Mose akatenga miji mitatu mashariki ya mto Yordani, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndipo Mose akatenga miji mitatu mashariki ya mto Yordani, Neno: Bibilia Takatifu Kisha Musa akatenga miji mitatu mashariki mwa Yordani, Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Musa akatenga miji mitatu mashariki ya Yordani, BIBLIA KISWAHILI Ndipo Musa akabagua miji mitatu ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki; |
Na hiyo miji mtakayowapa Walawi, itakuwa miji sita ya kukimbilia, mtakayoweka kwa ajili ya mwenye kumwua mtu, ili akimbilie huko; pamoja na hiyo mtawapa miji arubaini na miwili zaidi.
Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki.
itenge miji mitatu iwe kwako katikati ya nchi yako, akupayo BWANA, Mungu wako, kuimiliki.
ili kwamba amwuaye mtu apate kukimbilia huko, amwuaye jirani yake pasipo kujua, wala hakumchukia tangu hapo; ili apate kuishi akimbiliapo mmojawapo miji hiyo;