Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli.
Kumbukumbu la Torati 33:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akawa mfalme katika Yeshuruni, Walipokutanika wakuu wa watu, Makabila yote ya Israeli pamoja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu akawa mfalme wa Israeli, wakati viongozi wao walipokutana, na makabila yote yalipokusanyika. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu akawa mfalme wa Israeli, wakati viongozi wao walipokutana, na makabila yote yalipokusanyika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu akawa mfalme wa Israeli, wakati viongozi wao walipokutana, na makabila yote yalipokusanyika. Neno: Bibilia Takatifu Alikuwa mfalme juu ya Yeshuruni wakati viongozi wa watu walipokusanyika, pamoja na makabila ya Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Alikuwa mfalme juu ya Yeshuruni wakati viongozi wa watu walipokusanyika, pamoja na makabila ya Israeli. BIBLIA KISWAHILI Akawa mfalme katika Yeshuruni, Walipokutanika wakuu wa watu, Makabila yote ya Israeli pamoja. |
Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli.
wakiwa na neno, hunijia; nami naamua kati ya mtu na mwenziwe, nami nawajulisha amri za Mungu, na sheria zake.
Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao;
BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.
Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. BWANA, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme iko katikati yao.
Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake.
Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe.
Ndipo watu wa Israeli wakamwambia Gideoni, Tawala wewe juu yetu, wewe, na mwanao, na mjukuu wako pia; kwa kuwa wewe umetuokoa na mikono ya Midiani.
Haya, neneni tafadhali masikioni mwa wanaume wote wa Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi lililo bora kwenu, kwamba hao wana wa Yerubaali wote, ambao ni watu sabini, wawatawale, au kwamba mtu mmoja awatawale? Tena kumbukeni ya kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.