Kumbukumbu la Torati 33:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Musa alituagiza torati, Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose alituamuru tutii sheria; kitu cha thamani kuu cha taifa letu. Biblia Habari Njema - BHND Mose alituamuru tutii sheria; kitu cha thamani kuu cha taifa letu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose alituamuru tutii sheria; kitu cha thamani kuu cha taifa letu. Neno: Bibilia Takatifu sheria ile Musa aliyotupatia sisi, tulio milki ya kusanyiko la Yakobo. Neno: Maandiko Matakatifu sheria ile Musa aliyotupa sisi, tulio milki ya kusanyiko la Yakobo. BIBLIA KISWAHILI Musa alituagiza torati, Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo. |
Hizi ni amri, maagizo na sheria, BWANA alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.
Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
Je! Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua?
Msiliongeze neno ninalowaamuru wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, ninazowaamuru.