Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kumbukumbu la Torati 32:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

kulingana na idadi ya watoto wa Mungu, lakini alijiwekea watu wa Yakobo kuwa wake, hao alijichagulia kuwa mali yake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

kulingana na idadi ya watoto wa Mungu, lakini alijiwekea watu wa Yakobo kuwa wake, hao alijichagulia kuwa mali yake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

kulingana na idadi ya watoto wa Mungu, lakini alijiwekea watu wa Yakobo kuwa wake, hao alijichagulia kuwa mali yake.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa kuwa fungu la Mwenyezi Mungu ni watu wake, Yakobo kura yake ya urithi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa kuwa fungu la bwana ni watu wake, Yakobo kura yake ya urithi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kumbukumbu la Torati 32:9
28 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa mfalme atasikia, ili amwokoe mtumishi wake mkononi mwa yule mtu atakaye kuniharibu mimi na mwanangu pia katika urithi wa Mungu.


Mimi ni mmoja wa hao wenye amani, walio waaminifu katika Israeli; wewe unataka kuuharibu mji ulio kama mama wa Israeli; mbona unataka kuumeza urithi wa BWANA?


Kwa kuwa ni watu wako, na urithi wako, uliowatoa katika Misri, toka katikati ya tanuri ya chuma.


Kwa maana uliwatenga na watu wote wa dunia, wawe urithi wako, kama ulivyonena kwa mdomo wa Musa, mtumishi wako, hapo ulipowatoa baba zetu katika Misri, Ee Bwana MUNGU.


Hasira ya BWANA ikawaka juu ya watu wake, Akauchukia urithi wake.


Ili niuone wema wa wateule wako. Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako, Na kujisifu pamoja na watu wako.


Kwa sababu BWANA amejichagulia Yakobo, Na Israeli, wawe watu wake hasa.


Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako, Uwachunge, uwachukue milele.


Heri taifa ambalo BWANA ni Mungu wao, Watu aliowachagua kuwa urithi wake.


Ulikumbuke kusanyiko lako, Ulilolinunua zamani. Ulilolikomboa liwe kabila la urithi wako, Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.


Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa, Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake.


Hofu na woga zimewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee BWANA, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua.


Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.


kwa kuwa BWANA wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu.


Naye amewapigia kura, na mkono wake umewagawanyia kwa kamba; wataimiliki hata milele, watakaa ndani yake kizazi hata kizazi.


watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu.


Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila la urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.


Nami nikawatia katika nchi ya shibe, mpate kula matunda yake na mema yake; lakini ninyi mlipoingia katika nchi ile, mliitia unajisi nchi yangu, na urithi wangu mliufanya kuwa chukizo.


Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila la urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.


Kwa hiyo hamtakuwa na mtu atakayeitupa kamba kwa kura katika mkutano wa BWANA.


Na BWANA atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena.


macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;


Nao ni watu wako, urithi wako, uliowatoa kwa nguvu zako kuu na mkono wako ulionyoka.


kwa maana BWANA, Mungu wetu, yeye ndiye aliyetupandisha sisi na baba zetu kutoka nchi ya Misri; kutoka nyumba ya utumwa; naye ndiye aliyezifanya ishara zile kubwa mbele ya macho yetu, na kutulinda katika njia ile yote tuliyoiendea, na kati ya watu wa mataifa yote tuliopita katikati yao.


Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa kutoka kwa mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake.