Kumbukumbu la Torati 32:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana, mzabibu wao ni mzabibu wa Sodoma, Nao ni wa mashamba ya Gomora; Zabibu zao ni zabibu za uchungu, Vichala vyao ni vichungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana mizabibu yao ni miche ya Sodoma zimetoka katika konde za Gomora; zabibu zake ni zabibu zenye sumu, vishada vyake ni vichungu. Biblia Habari Njema - BHND Maana mizabibu yao ni miche ya Sodoma zimetoka katika konde za Gomora; zabibu zake ni zabibu zenye sumu, vishada vyake ni vichungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana mizabibu yao ni miche ya Sodoma zimetoka katika konde za Gomora; zabibu zake ni zabibu zenye sumu, vishada vyake ni vichungu. Neno: Bibilia Takatifu Mzabibu wao unatoka mzabibu wa Sodoma, na kutoka mashamba ya Gomora. Zabibu zake zimejaa sumu, na vishada vyake vimejaa uchungu. Neno: Maandiko Matakatifu Mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma, na kutoka kwenye mashamba ya Gomora. Zabibu zake zimejaa sumu, na vishada vyake vimejaa uchungu. BIBLIA KISWAHILI Maana, mzabibu wao ni mzabibu wa Sodoma, Nao ni wa mashamba ya Gomora; Zabibu zao ni zabibu za uchungu, Vichala vyao ni vichungu. |
Lisikieni neno la BWANA, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora.
Je! Ni kazi gani iliyohitajika kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi, nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibumwitu?
Nami nilikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibumwitu machoni pangu?
Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
Maana uovu wa binti ya watu wangu ni mkubwa Kuliko dhambi ya Sodoma, Uliopinduliwa kama katika dakika moja, Wala mikono haikuwekwa juu yake.
Lakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.
asiwe mtu katikati yenu, mume wala mke, wala jamaa, wala kabila, ageukaye moyo wake leo amwache BWANA, Mungu wetu, kwenda kuitumikia miungu ya mataifa hayo; lisiwe katikati yenu shina lizaalo uchungu na pakanga;
mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.