Naye atawatoa Israeli kwa ajili ya makosa ya Yeroboamu, aliyoyakosa, ambayo kwa hayo amewakosesha Israeli.
Kumbukumbu la Torati 32:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama BWANA asingaliwatoa? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mmoja anawezaje kuwashinda watu 1,000, au watu wawili wanawezaje kuwashinda watu 10,000, isipokuwa kama Mwamba wao amewatupa, Mwenyezi-Mungu wao amewaacha? Biblia Habari Njema - BHND Mtu mmoja anawezaje kuwashinda watu 1,000, au watu wawili wanawezaje kuwashinda watu 10,000, isipokuwa kama Mwamba wao amewatupa, Mwenyezi-Mungu wao amewaacha? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mmoja anawezaje kuwashinda watu 1,000, au watu wawili wanawezaje kuwashinda watu 10,000, isipokuwa kama Mwamba wao amewatupa, Mwenyezi-Mungu wao amewaacha? Neno: Bibilia Takatifu Mtu mmoja angewezaje kufukuza elfu moja, au wawili kufukuza elfu kumi, kama si kwamba Mwamba wao amewauza, kama si kwamba Mwenyezi Mungu amewaacha? Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mmoja angewezaje kufukuza elfu moja, au wawili kufukuza elfu kumi, kama si kwamba Mwamba wao amewauza, kama si kwamba bwana amewaacha? BIBLIA KISWAHILI Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama BWANA asingaliwatoa? |
Naye atawatoa Israeli kwa ajili ya makosa ya Yeroboamu, aliyoyakosa, ambayo kwa hayo amewakosesha Israeli.
Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kambi ya Washami, kumbe! Hapakuwa na mtu.
Hao Wagadi walikuwa makamanda wa jeshi, yeye aliyekuwa mdogo amelingana na mia moja, na yeye aliyekuwa mkuu, na elfu moja.
Maana wakaja jeshi la Washami watu wachache; BWANA akatia mikononi mwao jeshi kubwa mno, kwa sababu wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao. Hivyo wakamfanyia Yoashi hukumu.
Elfu moja watakimbia kwa kukemewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima.
BWANA asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.
Na watu watano wa kwenu watawafukuza watu mia moja, na watu mia moja wa kwenu watawafukuza watu elfu kumi; na adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga.
Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, ikalipwe ile deni.
Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.
Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia.
Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.
Kwa hiyo hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, naye akawauza na kuwatia mikononi mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia; na wana wa Israeli wakamtumikia huyo Kushan-rishathaimu muda wa miaka minane.
Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna yeyote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.