Ee BWANA, kwa ajili ya mtumishi wako, na kwa moyo wako mwenyewe, umeyatenda hayo makuu yote, ili yajulikane hayo matendo makuu yote.
Kumbukumbu la Torati 32:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana nitalitangaza Jina la BWANA; Mpeni ukuu Mungu wetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana nitalitangaza jina la Mwenyezi-Mungu, nanyi mseme, ‘Mungu wetu ni Mkuu’. Biblia Habari Njema - BHND Maana nitalitangaza jina la Mwenyezi-Mungu, nanyi mseme, ‘Mungu wetu ni Mkuu’. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana nitalitangaza jina la Mwenyezi-Mungu, nanyi mseme, ‘Mungu wetu ni Mkuu’. Neno: Bibilia Takatifu Nitalitangaza jina la Mwenyezi Mungu. Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu! Neno: Maandiko Matakatifu Nitalitangaza jina la bwana. Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu! BIBLIA KISWAHILI Maana nitalitangaza Jina la BWANA; Mpeni ukuu Mungu wetu. |
Ee BWANA, kwa ajili ya mtumishi wako, na kwa moyo wako mwenyewe, umeyatenda hayo makuu yote, ili yajulikane hayo matendo makuu yote.
Kwa hiyo Daudi akamhimidi BWANA, mbele ya mkutano wote; naye Daudi akasema, Uhimidiwe, Ee BWANA, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele.
Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo wako, na ng'ombe wako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.
Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.
nami nilimtokea Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Ee BWANA; wewe ndiwe uliye mkuu, na jina lako ni kuu katika uweza.
Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu.
Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Nami niliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.
Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.
na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;
Ee BWANA Mungu, umeanza kumwonesha mtumishi wako ukubwa wako, na mkono wako wa nguvu; kwani kuna mungu gani mbinguni au duniani awezaye kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa matendo yako yenye nguvu?
mkasema, Tazama, BWANA, Mungu wetu, ametuonesha utukufu wake, na ukuu wake, nasi tunasikia sauti yake toka kati ya moto; mmeona leo ya kuwa Mungu husema na mwanadamu, naye akaishi.
Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.