Kumbukumbu la Torati 32:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nilisema, Ningewatawanyia mbali, Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilisema, ningaliwaangamiza kabisa na kuwafanya wasikumbukwe tena na mtu yeyote, Biblia Habari Njema - BHND Nilisema, ningaliwaangamiza kabisa na kuwafanya wasikumbukwe tena na mtu yeyote, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilisema, ningaliwaangamiza kabisa na kuwafanya wasikumbukwe tena na mtu yeyote, Neno: Bibilia Takatifu Nilisema ningewatawanya na kufuta kumbukumbu lao katika mwanadamu. Neno: Maandiko Matakatifu Nilisema ningewatawanya na kufuta kumbukumbu lao katika mwanadamu. BIBLIA KISWAHILI Nilisema, Ningewatawanyia mbali, Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu; |
Kwa nini Wamisri waseme, kuwa “Amewatoa ili awatende mabaya, apate kuwaua milimani na kuwaangamiza watoke juu ya uso wa nchi?” Geuza katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.
Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu.
Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Abrahamu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.
Nanyi nitawatapanyatapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ni ukiwa, na miji yenu maganjo.
Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hadi majira ya Mataifa yatakapotimia.
BWANA atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huku na huko katika falme zote za duniani.
Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA.
BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe.
Na BWANA atawatawanya kati ya mataifa, nanyi mtasalia watu wachache kati ya makabila, mtakakopelekwa mbali na BWANA.
niache, nipate kuwaangamiza, na kulifuta jina lao chini ya mbingu; nami nitakufanya wewe uwe taifa kubwa lenye nguvu kuliko wao.