Kumbukumbu la Torati 32:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nitaweka madhara juu yao chungu chungu; Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitarundika maafa chungu nzima juu yao, nitawamalizia mishale yangu. Biblia Habari Njema - BHND Nitarundika maafa chungu nzima juu yao, nitawamalizia mishale yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitarundika maafa chungu nzima juu yao, nitawamalizia mishale yangu. Neno: Bibilia Takatifu “Nitalundika majanga juu yao na kutumia mishale yangu dhidi yao. Neno: Maandiko Matakatifu “Nitalundika majanga juu yao na kutumia mishale yangu dhidi yao. BIBLIA KISWAHILI Nitaweka madhara juu yao chungu chungu; Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe; |
kwa sababu wameniacha mimi, wameifukizia uvumba miungu mingine, ili wapate kunikasirisha kwa kazi yote ya mikono yao; kwa hiyo hasira yangu itawaka juu ya mahali hapa, isizimike.
Umeliongeza hilo taifa, BWANA, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.
Maana Bwana MUNGU asema hivi; Je! U zaidi sana nitakapoleta hukumu zangu nne zilizo kali juu ya Yerusalemu, yaani, upanga, na njaa, na wanyama wabaya, na tauni, niwakatilie mbali nayo wanadamu na wanyama?
hapo nitakapoiachilia mishale mibaya ya njaa juu yao, mishale iletayo uharibifu nitakayoiachilia ili kuwaharibu ninyi; nami nitaiongeza njaa juu yenu, na tegemeo lenu la mkate nitalivunja.
Waueni kabisa, wazee, na viijana, na wasichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.
Tena ikiwa baada ya hayo hamtaki kunisikiza, ndipo nitawaadhibu zaidi mara saba kwa ajili ya dhambi zenu.
Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
BWANA atamtenga kwa uovu, kutoka kabila zote za Israeli, kwa laana zote za agano lililoandikwa katika kitabu hiki cha torati.
Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui.