Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, Na mwenye choyo humkana BWANA na kumdharau.
Kumbukumbu la Torati 32:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA akaona, akawachukia, Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu aliona jambo hilo akawaacha; aliwakataa watoto wake, waume kwa wake. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu aliona jambo hilo akawaacha; aliwakataa watoto wake, waume kwa wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu aliona jambo hilo akawaacha; aliwakataa watoto wake, waume kwa wake. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akaona hili, akawakataa, kwa sababu alikasirishwa na wanawe wa kiume na wa kike. Neno: Maandiko Matakatifu bwana akaona hili, akawakataa, kwa sababu alikasirishwa na wanawe na binti zake. BIBLIA KISWAHILI BWANA akaona, akawachukia, Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake. |
Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, Na mwenye choyo humkana BWANA na kumdharau.
Sikieni, enyi mbingu, tega sikio, Ee nchi, kwa maana BWANA amenena; Nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi.
Mpenzi wangu afanya nini nyumbani mwangu, ikiwa amefanya uasherati? Je! Nadhiri zako na nyama takatifu zitakuondolea hatia? Ufanyapo maovu, ndipo uonapo furaha.
Naye mkuu wa askari walinzi akamtwaa Yeremia, akamwambia, BWANA, Mungu wako, alitamka mabaya haya juu ya mahali hapa;
Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu, Kana kwamba ni ya bustani tu; Ameziharibu sikukuu zake; BWANA amezisahaulisha katika Sayuni Sikukuu na sabato; Naye amewadharau mfalme na kuhani Katika uchungu wa hasira yake.
Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia.
Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema BWANA, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.
Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.
Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.