Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arubaini, hata walipofikia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikia mipakani mwa nchi ya Kanaani.
Kumbukumbu la Torati 29:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC lakini BWANA hakuwapa moyo wa kujua, wala macho ya kuona, wala masikio ya kusikia, hata leo hivi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mpaka leo Mwenyezi-Mungu hajawapa akili ya kuelewa, macho ya kuona, wala masikio ya kusikia! Biblia Habari Njema - BHND Lakini mpaka leo Mwenyezi-Mungu hajawapa akili ya kuelewa, macho ya kuona, wala masikio ya kusikia! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mpaka leo Mwenyezi-Mungu hajawapa akili ya kuelewa, macho ya kuona, wala masikio ya kusikia! Neno: Bibilia Takatifu Lakini hadi leo Mwenyezi Mungu hajawapa akili ya kuelewa au macho yanayoona au masikio yanayosikia. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini mpaka leo bwana hajawapa akili ya kuelewa au macho yanayoona au masikio yanayosikia. BIBLIA KISWAHILI lakini BWANA hakuwapa moyo wa kujua, wala macho ya kuona, wala masikio ya kusikia, hata leo hivi. |
Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arubaini, hata walipofikia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikia mipakani mwa nchi ya Kanaani.
Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanya kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, makabila ya urithi wako.
Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.
Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.
ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wametengwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;
Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alifanya roho yake kuwa ngumu, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate kumtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo.
Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, amekubariki katika kazi yote ya mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arubaini hii alikuwa nawe BWANA, Mungu wako; hukukosa kitu.
akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awajalie ili watubu na kuijua kweli;