Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, kisha mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, na wenye ujasiri.
Kumbukumbu la Torati 27:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “ ‘Alaaniwe mtu yeyote anayeua mtu kwa siri’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ Biblia Habari Njema - BHND “ ‘Alaaniwe mtu yeyote anayeua mtu kwa siri’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “‘Alaaniwe mtu yeyote anayeua mtu kwa siri’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ Neno: Bibilia Takatifu “Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” Neno: Maandiko Matakatifu “Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” BIBLIA KISWAHILI Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina. |
Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, kisha mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, na wenye ujasiri.
Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hadi katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hadi akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake.
Na zaidi ya hayo, unajua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua, na kumwaga damu wakati wa amani akilipiza kisasi cha vita, mshipi akautia damu ya vita uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake.
Mtu yeyote atakayemwua mtu, huyo mwuaji atauawa kwa vinywa vya mashahidi; lakini shahidi mmoja hatashuhudia juu ya mtu akauliwa.
Tena, msipokee fidia kwa ajili ya uhai wa mwuaji, ambaye amekuwa na hatia ya mauti; Lakini lazima atauawa.