Kisha akawaambia, Nendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyekuwa na kitu; maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.
Kumbukumbu la Torati 26:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC ukayafurahie mema yote ambayo BWANA, Mungu wako, amekupa, na nyumba yako, wewe, na Mlawi, na mgeni aliye kati yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nawe utafurahia mema yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amekujalia wewe na jamaa yako. Nao watafurahi pamoja nawe. Biblia Habari Njema - BHND Nawe utafurahia mema yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amekujalia wewe na jamaa yako. Nao watafurahi pamoja nawe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nawe utafurahia mema yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amekujalia wewe na jamaa yako. Nao watafurahi pamoja nawe. Neno: Bibilia Takatifu Kisha wewe pamoja na Walawi na wageni wote walio miongoni mwenu mtafurahi katika vitu vyote vizuri ambavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewapa pamoja na wa nyumbani mwenu. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha wewe pamoja na Walawi na wageni wote walioko miongoni mwenu mtafurahi katika vitu vyote vizuri ambavyo bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa pamoja na wa nyumbani mwenu. BIBLIA KISWAHILI ukayafurahie mema yote ambayo BWANA, Mungu wako, amekupa, na nyumba yako, wewe, na Mlawi, na mgeni aliye kati yako. |
Kisha akawaambia, Nendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyekuwa na kitu; maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.
Mimi najua ya kwamba hakuna jema kwao kupita kufurahi, na kufanya mema maadamu wanaishi.
Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.
Tazama, mimi niliyoyaona kuwa ndiyo mema na ya kufaa, ni mtu kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote anayoifanya chini ya jua, siku zote za maisha yake alizopewa na Mungu; maana hilo ndilo fungu lake.
Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lolote litakalofuata baada yake.
tazama, watumishi wangu wataimba kwa furaha ya moyo, bali ninyi mtalia kwa huzuni ya moyo; mtapiga kelele kwa sababu ya uchungu wa roho zenu.
Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake.
Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?
Nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, ninyi, na wana wenu, na binti zenu, na watumishi wenu wa kiume na wa kike, na Mlawi aliyemo malangoni mwenu; kwa kuwa hana sehemu wala urithi kwenu.
lakini hivyo mtakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, wewe, na mwanao wa kiume na wa kike, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako.
na huko mtakula mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi furahini katika yote mtakayotia mikono yenu, ninyi na wa nyumbani mwenu, aliyokubarikia BWANA, Mungu wako.
nawe utafurahi mbele ya BWANA, Mungu wako, wewe na mwana wako na binti yako, na mtumwa wako na mjakazi wako, na Mlawi aliye ndani ya malango yako, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio katikati yako, katika mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake.
kwa kuwa hukumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote;