Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.
Kumbukumbu la Torati 26:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na sasa, tazama, nimeleta malimbuko ya mazao ya ardhi uliyonipa, Ee BWANA. Kisha ukiweke chini mbele za BWANA, Mungu wako, ukasujudu mbele za BWANA, Mungu wako; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Na sasa ninamletea Mwenyezi-Mungu malimbuko ya mazao ya nchi ambayo amenipa.’ “Kisha utaweka kikapu chini, mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na kuabudu mbele zake. Biblia Habari Njema - BHND Na sasa ninamletea Mwenyezi-Mungu malimbuko ya mazao ya nchi ambayo amenipa.’ “Kisha utaweka kikapu chini, mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na kuabudu mbele zake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Na sasa ninamletea Mwenyezi-Mungu malimbuko ya mazao ya nchi ambayo amenipa.’ “Kisha utaweka kikapu chini, mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na kuabudu mbele zake. Neno: Bibilia Takatifu nami sasa ninaleta malimbuko ya ardhi ambayo wewe, Ee Mwenyezi Mungu, umenipa.” Weka kapu mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na usujudu mbele zake. Neno: Maandiko Matakatifu nami sasa ninaleta malimbuko ya ardhi ambayo wewe, Ee bwana, umenipa.” Weka kapu mbele za bwana Mwenyezi Mungu wako na usujudu mbele zake. BIBLIA KISWAHILI Na sasa, tazama, nimeleta malimbuko ya mazao ya ardhi uliyonipa, Ee BWANA. Kisha ukiweke chini mbele za BWANA, Mungu wako, ukasujudu mbele za BWANA, Mungu wako; |
Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.
Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.
Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, Humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake,
Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao wanaume utanipa mimi.
Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.
Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru; kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.
Malimbuko ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo wako, umpe.
Umemwungama BWANA leo, kuwa ndiye Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake, na kushika amri zake na maagizo yake, na hukumu zake, na kusikiza sauti yake;
twaa malimbuko ya ardhi, utakayoyavuna katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako; ukayatie katika kikapu, ukaende hata mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wako, ili alikalishe jina lake huko.
Naye kuhani atakipokea kikapu mkononi mwako, akiweke chini mbele ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako.
Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.