Kumbukumbu la Torati 24:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwizi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mtu yeyote akimwiba Mwisraeli mwenzake na kumfanya mtumwa wake au kumwuza utumwani, mtu huyo lazima auawe. Ndivyo mtakavyokomesha uovu miongoni mwenu. Biblia Habari Njema - BHND “Mtu yeyote akimwiba Mwisraeli mwenzake na kumfanya mtumwa wake au kumwuza utumwani, mtu huyo lazima auawe. Ndivyo mtakavyokomesha uovu miongoni mwenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mtu yeyote akimwiba Mwisraeli mwenzake na kumfanya mtumwa wake au kumwuza utumwani, mtu huyo lazima auawe. Ndivyo mtakavyokomesha uovu miongoni mwenu. Neno: Bibilia Takatifu Kama mtu akikamatwa akiiba yeyote miongoni mwa ndugu zake wa Waisraeli na kumtenda kama mtumwa au akimuuza, mwizi huyo ni lazima auawe. Nawe utaondoa uovu kutoka miongoni mwenu. Neno: Maandiko Matakatifu Kama mtu akikamatwa akiiba yeyote miongoni mwa ndugu zake wa Waisraeli na kumtenda kama mtumwa au akimuuza, mwizi huyo ni lazima auawe. Nawe utaondoa uovu kutoka miongoni mwenu. BIBLIA KISWAHILI Mtu akionekana anamwiba nduguye mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwizi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. |
Ugiriki na Tubali na Mesheki ndio waliokuwa wachuuzi wako; walitoa wanadamu, na vyombo vya shaba, kwa biashara yako.
Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mama yako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako;
Mikono ya wale mashahidi na iwe juu yake kwanza kwa kumwua, kisha mikono ya watu wote. Uondoe vivyo hivyo uovu katikati yako.
ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani.
na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na linginelo lolote lisilopatana na mafundisho ya kweli;
na mdalasini, iliki, uvumba, marhamu, ubani, mvinyo, mafuta ya mzeituni, unga mzuri na ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari, na miili na roho za wanadamu.