Kumbukumbu la Torati 24:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Usimdhulumu kibarua maskini na mhitaji, awe Mwisraeli au mmoja wa wageni wanaoishi katika miji yenu. Biblia Habari Njema - BHND “Usimdhulumu kibarua maskini na mhitaji, awe Mwisraeli au mmoja wa wageni wanaoishi katika miji yenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Usimdhulumu kibarua maskini na mhitaji, awe Mwisraeli au mmoja wa wageni wanaoishi katika miji yenu. Neno: Bibilia Takatifu Usimwonee mtu maskini na mhitaji ambaye umemwajiri, akiwa ni nduguyo Mwisraeli au mgeni anayeishi katika mojawapo ya miji yenu. Neno: Maandiko Matakatifu Usimwonee mtu maskini na mhitaji ambaye umemwajiri, akiwa ni nduguyo Mwisraeli au mgeni anayeishi katika mojawapo ya miji yenu. BIBLIA KISWAHILI Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako; |
Ndani yako wamedharau baba na mama; kati yako wamewatenda wageni udhalimu; ndani yako wamewaonea yatima na mjane.
Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang'anya mali yake; ujira wake aliyeajiriwa usikae kwako usiku kucha hadi asubuhi.
nao hukanyaga vichwa vya maskini katika mavumbi ya nchi na kuwasukuma walioteseka kutoka kwa njia yao; na mtu na baba yake wanamwendea mwanamke mmoja, na kulitia unajisi jina langu takatifu;
Lisikieni neno hili, enyi ng'ombe wa Bashani, mnaokaa juu ya mlima wa Samaria, mnaowaonea maskini, na kuwaponda wahitaji; mnaowaambia bwana zao, Haya! Leteni, tunywe.
Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.
Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mfanya kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihamahame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini;
Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.