Na Yehoshafati akakaa Yerusalemu; akatoka tena kwenda kati ya watu toka Beer-sheba mpaka milima ya Efraimu, akawarudisha kwa BWANA, Mungu wa baba zao.
Kumbukumbu la Torati 23:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Utakapotoka kwenda juu ya adui zako nawe u katika kambi, jilinde na kila neno baya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mkienda vitani, mkapiga kambi, kila mmoja ajihadhari na kitu chochote kiovu. Biblia Habari Njema - BHND “Mkienda vitani, mkapiga kambi, kila mmoja ajihadhari na kitu chochote kiovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mkienda vitani, mkapiga kambi, kila mmoja ajihadhari na kitu chochote kiovu. Neno: Bibilia Takatifu Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu chochote kisicho safi. Neno: Maandiko Matakatifu Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu chochote kisicho safi. BIBLIA KISWAHILI Utakapotoka kwenda juu ya adui zako nawe u katika kambi, jilinde na kila neno baya. |
Na Yehoshafati akakaa Yerusalemu; akatoka tena kwenda kati ya watu toka Beer-sheba mpaka milima ya Efraimu, akawarudisha kwa BWANA, Mungu wa baba zao.
Na hivyo ndivyo alivyofanya Hezekia katika Yuda yote; akatenda yaliyo mema, na ya adili, na uaminifu, mbele za BWANA, Mungu wake.
Wala mgeni, aambatanaye na BWANA, asiseme hivi, Hakika yake BWANA atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu.
Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtosheke na mishahara yenu.
Akiwa kwenu mtu awaye yote asiyekuwa ni tohara kwa ajili ya yaliyomtukia usiku, na atoke nje ya kituo, wala asiingie ndani ya kituo;
Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtaifanya kambi ya Israeli kuwa imelaaniwa na kuifadhaisha.
Ndipo wana wa Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea, wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za BWANA, wakafunga siku hiyo hadi jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.