Kumbukumbu la Torati 22:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utamwacha mamandege aende zake, lakini unaweza kuchukua makinda. Ukifanya hivyo utafanikiwa na kuishi maisha marefu. Biblia Habari Njema - BHND Utamwacha mamandege aende zake, lakini unaweza kuchukua makinda. Ukifanya hivyo utafanikiwa na kuishi maisha marefu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utamwacha mamandege aende zake, lakini unaweza kuchukua makinda. Ukifanya hivyo utafanikiwa na kuishi maisha marefu. Neno: Bibilia Takatifu Unaweza kuchukua makinda, lakini hakikisha unamwachilia huyo ndege, ili upate kufanikiwa na kuishi maisha marefu. Neno: Maandiko Matakatifu Waweza kuchukua makinda, lakini uwe na hakika ya kumwacha huyo ndege, ili upate kufanikiwa na uweze kuishi maisha marefu. BIBLIA KISWAHILI sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi. |
Utakapojenga nyumba mpya, fanya ukuta kandokando ya dari lako, usije ukaleta damu juu ya nyumba yako, mtu akianguka huko.
Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo BWANA, Mungu wako, milele.
Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.