Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nilikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.
Kumbukumbu la Torati 22:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu mume asimtwae mke wa baba yake, wala asifunue ncha ya mavazi ya baba yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mwanamume yeyote kamwe asilale na mke wa baba yake. Biblia Habari Njema - BHND “Mwanamume yeyote kamwe asilale na mke wa baba yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mwanamume yeyote kamwe asilale na mke wa baba yake. Neno: Bibilia Takatifu Mwanaume asimwoe mke wa baba yake; kamwe asidhalilishe kitanda cha baba yake. Neno: Maandiko Matakatifu Mwanaume asimwoe mke wa baba yake; kamwe asidhalilishe kitanda cha baba yake. BIBLIA KISWAHILI Mtu mume asimtwae mke wa baba yake, wala asifunue ncha ya mavazi ya baba yake. |
Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nilikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.
Na mwanamume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
Hakika habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.
yule mwanamume aliyelala naye na ampe baba yake yule binti shekeli hamsini za fedha, kisha na awe mkewe, kwa kuwa amemtweza; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote.
Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.
Akasema, Ama! Ni nani wewe? Akamjibu, Ni mimi, Ruthu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu.