Hata baadaye Daudi aliposikia, akasema, Mimi na ufalme wangu hatuna hatia milele mbele za BWANA, kwa sababu ya damu ya Abneri, mwana wa Neri;
Kumbukumbu la Torati 21:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee BWANA, wasamehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mwenyezi-Mungu, uwasamehe watu wako wa Israeli ambao umewakomboa, usiwawekee watu wako Israeli hatia ya mauaji ya mtu asiye na hatia, ila uwasamehe hatia hiyo.’ Biblia Habari Njema - BHND Ee Mwenyezi-Mungu, uwasamehe watu wako wa Israeli ambao umewakomboa, usiwawekee watu wako Israeli hatia ya mauaji ya mtu asiye na hatia, ila uwasamehe hatia hiyo.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mwenyezi-Mungu, uwasamehe watu wako wa Israeli ambao umewakomboa, usiwawekee watu wako Israeli hatia ya mauaji ya mtu asiye na hatia, ila uwasamehe hatia hiyo.’ Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, ukubali upatanisho kwa watu wako Israeli ambao umewakomboa, wala usiwahesabie watu wako hatia ya damu ya mtu asiyekuwa na hatia.” Nayo damu iliyomwagika itakuwa imefanyiwa upatanisho. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, ukubali upatanisho kwa watu wako Israeli, ambao umewakomboa, wala usiwahesabie watu wako hatia ya damu ya mtu asiyekuwa na hatia.” Nayo damu iliyomwagika itakuwa imefanyiwa upatanisho. BIBLIA KISWAHILI Ee BWANA, wasamehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwayo. |
Hata baadaye Daudi aliposikia, akasema, Mimi na ufalme wangu hatuna hatia milele mbele za BWANA, kwa sababu ya damu ya Abneri, mwana wa Neri;
Mfalme akamwambia, Fanya alivyonena, umpige, ukamzike; ili uniondolee mimi na nyumba ya babangu damu aliyoimwaga Yoabu bure.
tena kwa ajili ya damu zisizo na hatia alizozimwaga; kwani aliujaza Yerusalemu damu zisizo na hatia; wala BWANA hakukubali kusamehe.
Lakini jueni hakika kwamba, mkiniua, mtajiletea juu yenu damu isiyo na hatia itakuwa juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake; kwa maana ni kweli BWANA amenituma kwenu, kuwaambieni yote mliyoyasikia.
nao walizini huko Misri; walizini wakati wa ujana wao; huko vifua vyao vilishikwashikwa, na matiti yao yakatomaswa wakapoteza ubikira wao.
wala hamleti mlangoni pa hema ya kukutania, kama matoleo kwa BWANA mbele ya hema ya BWANA; mtu huyo atahesabiwa kuwa ana hatia ya damu; amemwaga damu; na atatupiliwa mbali na watu wake;
Basi wakamlilia BWANA, wakasema, Twakuomba, Ee BWANA, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, BWANA, umefanya kama ulivyopenda.
hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.