Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.
Kumbukumbu la Torati 2:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hivi leo ivuke Ari, mpaka wa Moabu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema ‘Leo hii mtauvuka mpaka wa Moabu kwa kupitia nchi ya Ari. Biblia Habari Njema - BHND ‘Leo hii mtauvuka mpaka wa Moabu kwa kupitia nchi ya Ari. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza ‘Leo hii mtauvuka mpaka wa Moabu kwa kupitia nchi ya Ari. Neno: Bibilia Takatifu “Leo utapita katika nchi ya Moabu huko Ari. Neno: Maandiko Matakatifu “Leo utapita katika nchi ya Moabu huko Ari. BIBLIA KISWAHILI Hivi leo ivuke Ari, mpaka wa Moabu; |
Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.
Kutoka huko wakasafiri, wakapanga upande wa pili wa Arnoni, ulio jangwani, utokao katika mpaka wa Waamori; maana, Arnoni ndio mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.
Na materemko ya hizo bonde Kwenye kuteremkia maskani ya Ari, Na kutegemea mpaka wa Moabu.
Lakini Sihoni hakukubali kumwacha Israeli kupita katika mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, akatoka aende kupigana na Israeli jangwani, akafika mpaka Yahasa; akapigana na Israeli.
BWANA akaniambia, Usiwasumbue Wamoabi, wala usishindane nao katika mapigano; kwa kuwa sitakupa katika nchi yake kuimiliki; kwa sababu Ari nimewapa wana wa Lutu kuimiliki.
Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki mwa nchi ya Moabu, wakapiga kambi upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu.