Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.
Kumbukumbu la Torati 18:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Wamesema ukweli. Biblia Habari Njema - BHND Naye Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Wamesema ukweli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Wamesema ukweli. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akaniambia: “Wanachosema ni vyema. Neno: Maandiko Matakatifu bwana akaniambia: “Wanachosema ni vyema. BIBLIA KISWAHILI BWANA akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema. |
Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.
Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;
Mimi niwaiwanulia nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
Sasa basi, mbona tufe? Maana moto huu mkubwa utatuteketeza; tukiisikia tena sauti ya BWANA, Mungu wetu, tutakufa.
Naye BWANA akasikia sauti ya maneno yenu mliyoniambia; BWANA akaniambia, Nimesikia sauti ya maneno ya watu hawa waliyokuambia; wamesema vema yote waliyosema.