Kisha Shafani mwandishi akamwambia mfalme, akasema, Hilkia kuhani amenipa kitabu. Shafani akakisoma mbele ya mfalme.
Kumbukumbu la Torati 17:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nakala hiyo atakuwa nayo daima na kuisoma maisha yake yote, ili apate kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, akishika na kutimiza maneno yote ya sheria hii na masharti haya, Biblia Habari Njema - BHND Nakala hiyo atakuwa nayo daima na kuisoma maisha yake yote, ili apate kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, akishika na kutimiza maneno yote ya sheria hii na masharti haya, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nakala hiyo atakuwa nayo daima na kuisoma maisha yake yote, ili apate kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, akishika na kutimiza maneno yote ya sheria hii na masharti haya, Neno: Bibilia Takatifu Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili ajifunze kumheshimu Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi, Neno: Maandiko Matakatifu Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili kwamba ajifunze kumheshimu bwana Mwenyezi Mungu wake na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi, BIBLIA KISWAHILI na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya; |
Kisha Shafani mwandishi akamwambia mfalme, akasema, Hilkia kuhani amenipa kitabu. Shafani akakisoma mbele ya mfalme.
Mnayachunguza maandiko kwa sababu mnadhani kuwa ndani yake ninyi mna uzima wa milele; na maandiko yayo hayo ndiyo yanayonishuhudia.
Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu.
siku ile uliyosimama mbele za BWANA wako huko Horebu, BWANA aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawafanya wasikilize maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao.
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;
Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu nisemazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuzizingatia.
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.