Katika siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja Pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile Pasaka?
Kumbukumbu la Torati 16:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usimchinje Pasaka ndani ya malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msitolee sadaka ya Pasaka katika mji wowote ambao Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawapa, Biblia Habari Njema - BHND Msitolee sadaka ya Pasaka katika mji wowote ambao Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawapa, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msitolee sadaka ya Pasaka katika mji wowote ambao Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawapa, Neno: Bibilia Takatifu Kamwe msitoe dhabihu ya Pasaka katika mji wowote ambao Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewapa, Neno: Maandiko Matakatifu Kamwe msitoe dhabihu ya Pasaka katika mji wowote ambao bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa, BIBLIA KISWAHILI Usimchinje Pasaka ndani ya malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako; |
Katika siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja Pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile Pasaka?
Nawe umchinjie Pasaka BWANA, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake.
Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale chochote usiku kucha hata asubuhi.
ila mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, ndipo mtakapomchinja Pasaka jioni, katika machweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka Misri.