Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida.
Kumbukumbu la Torati 15:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Waweza kumtoza mgeni; lakini kila uwiacho kwa nduguyo mkono wako utamwachilia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mnaweza kuwadai wageni, lakini madeni yote ya ndugu zenu wenyewe mtayafuta. Biblia Habari Njema - BHND Mnaweza kuwadai wageni, lakini madeni yote ya ndugu zenu wenyewe mtayafuta. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mnaweza kuwadai wageni, lakini madeni yote ya ndugu zenu wenyewe mtayafuta. Neno: Bibilia Takatifu Unaweza kudai malipo kwa mgeni, lakini lazima ufute kila deni ambalo unamdai ndugu yako. Neno: Maandiko Matakatifu Unaweza kudai malipo kwa mgeni, lakini lazima ufute kila deni ambalo unamdai ndugu yako. BIBLIA KISWAHILI Waweza kumtoza mgeni; lakini kila uwiacho kwa nduguyo mkono wako utamwachilia. |
Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida.
Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Na jinsi ya maachilio ni hii, kila mkopeshaji na akiache alichomkopesha mwenziwe, wala asimlipize mwenziwe wala nduguye; kwa kuwa imepigwa mbiu ya maachilio ya BWANA.
mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.
Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.