Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Abrahamu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.
Kumbukumbu la Torati 15:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawe utakapomwacha huru aondoke kwako, usimwache aende zake mikono mitupu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nawe utakapomwacha huru, usimwache aende mikono mitupu. Biblia Habari Njema - BHND Nawe utakapomwacha huru, usimwache aende mikono mitupu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nawe utakapomwacha huru, usimwache aende mikono mitupu. Neno: Bibilia Takatifu Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu. Neno: Maandiko Matakatifu Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu. BIBLIA KISWAHILI Nawe utakapomwacha huru aondoke kwako, usimwache aende zake mikono mitupu; |
Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Abrahamu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.
Nami nitawapa watu hao kufadhiliwa mbele ya Wamisri; hata itakuwa, hapo mtakapokwenda zenu hamtakwenda kitupu;
Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu! Na vyumba vyake kwa udhalimu! Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira, Wala hampi mshahara wake;
Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.
Ikiwa nduguyo, mume wa Kiebrania, au mwanamke wa Kiebrania, akiuzwa kwako, naye amekutumikia miaka sita; basi mwaka wa saba mwache huru aondoke kwako.
umwangalie kwa wema katika kundi lako, na sakafu yako ya nafaka, na kinu chako cha divai; mpe kama alivyokubarikia BWANA, Mungu wako.
Ninyi akina bwana, wapeni watumishi wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.