Wajua kuwa Daudi baba yangu hakuweza kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata BWANA alipowatia watu chini ya nyayo zake.
Kumbukumbu la Torati 14:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kulungu, paa, kongoni, mbuzimwitu, paa mweupe, pofu na mbuzi wa mlimani; Biblia Habari Njema - BHND kulungu, paa, kongoni, mbuzimwitu, paa mweupe, pofu na mbuzi wa mlimani; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kulungu, paa, kongoni, mbuzimwitu, paa mweupe, pofu na mbuzi wa mlimani; Neno: Bibilia Takatifu kulungu, paa, kongoni, paa mweupe, mbuzi-mwitu, pofu na kondoo wa mlimani. Neno: Maandiko Matakatifu kulungu, paa, kongoni, paa mweupe, mbuzi-mwitu, pofu na kondoo wa mlimani. BIBLIA KISWAHILI kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima; |
Wajua kuwa Daudi baba yangu hakuweza kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata BWANA alipowatia watu chini ya nyayo zake.
Je! Wajua majira ya kuzaa kwao mbuzi-mwitu walio majabalini? Au waweza kusema majira ya kuzaa kwa kulungu?
Wana wako wamezimia, Wamelala penye pembe za njia kuu zote Kama kulungu wavuni; Wamejaa hasira ya BWANA, Lawama ya Mungu wako.
Pamoja na haya, waweza kuchinja nyama na kula ndani ya malango yako yote, kwa kufuata yote yanayotamaniwa na roho yako, kulingana na baraka ya BWANA, Mungu wako, aliyokupa; aliye tohara na asiye tohara ana ruhusa kula katika nyama hiyo, kama ya paa na ya kulungu.
Kama vile anavyoliwa paa na kulungu, ndivyo utakavyoila nyama hii; asiyekuwa tohara na aliye tohara wataila pia.
na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla.