Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Kumbukumbu la Torati 14:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika mavuno yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Toeni sehemu moja ya kumi ya mazao yenu yote ya shambani kila mwaka. Biblia Habari Njema - BHND “Toeni sehemu moja ya kumi ya mazao yenu yote ya shambani kila mwaka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Toeni sehemu moja ya kumi ya mazao yenu yote ya shambani kila mwaka. Neno: Bibilia Takatifu Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka. Neno: Maandiko Matakatifu Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka. BIBLIA KISWAHILI Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika mavuno yote ya mbegu zako, yatokayo shambani mwaka baada ya mwaka. |
Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Wakati wa mavuno mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakaposalia zitakuwa zenu wenyewe, kuwa mbegu za nchi, na chakula chenu, na chakula chao waliomo nyumbani mwenu, na chakula cha watoto wenu.
Yusufu akaifanya kuwa sheria ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao.
tena tuyalete malimbuko ya unga wetu, na matoleo yetu, na matunda ya miti ya namna zote, mvinyo, na mafuta, kwa makuhani, hapo vyumbani kwa nyumba ya Mungu wetu; na zaka za ardhi yetu kwa Walawi; kwa kuwa hao Walawi ndio wanaozitwaa zaka vijijini kwetu kote.
Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Kutoka kwa unga wenu mtakaokanda kwanza wa chengachenga mtasongeza sadaka ya unga wa kuinuliwa uwe sadaka ya kuinuliwa; vile vile kama mfanyavyo sadaka ya kuinuliwa ya sakafu ya kupuchukulia nafaka, ndivyo mtakavyoiinua.
Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.
Nanyi mtakula hayo kila mahali, ninyi na watu wa nyumbani mwenu; kwa kuwa ni thawabu yenu badala ya utumishi wenu katika hema ya kukutania.
Usile ndani ya makazi yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng'ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zozote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako;
pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng'ombe na ya kondoo;