na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.
Kumbukumbu la Torati 12:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Neno lolote ninalowaagiza lizingatieni, usilizidishe, wala usilipunguze. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Hakikisheni kwamba mmefanya kila kitu nilichowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu. Biblia Habari Njema - BHND “Hakikisheni kwamba mmefanya kila kitu nilichowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Hakikisheni kwamba mmefanya kila kitu nilichowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu. Neno: Bibilia Takatifu Hakikisheni kwamba mnafanya yote niliyowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu. Neno: Maandiko Matakatifu Angalieni kwamba mnafanya yote niliyowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu. BIBLIA KISWAHILI Neno lolote ninalowaagiza lizingatieni, usilizidishe, wala usilipunguze. |
na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.
BWANA akaniambia, Mwanadamu, weka moyoni mwako, ukatazame kwa macho yako, ukasikie kwa masikio yako, maneno yote nitakayokuambia, katika habari ya kawaida zote za nyumba ya BWANA, na ya amri zake zote; nawe weka moyoni mwako maingilio ya nyumba, pamoja na matokeo yote ya mahali patakatifu.
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
utakaposikiza sauti ya BWANA, Mungu wako kwa kushika maagizo yake yote nikuagizayo leo, ufanye yaliyoelekea machoni pa BWANA, Mungu wako.
nawe ukiyashika maagizo haya yote nikuagizayo leo, na kuyafanya, kumpenda BWANA, Mungu wako, na kwenda sikuzote katika njia zake, ndipo ujiongezee miji mitatu tena, pamoja na mitatu ile;
Msiliongeze neno ninalowaamuru wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, ninazowaamuru.
Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda kulingana na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kulia, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.