Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA akaiendea njia ya Yeroboamu, na kosa lake ambalo kwa hilo aliwakosesha Israeli.
Kumbukumbu la Torati 12:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jihadharini msitoe sadaka zenu za kuteketezwa mahali popote mnapopaona; Biblia Habari Njema - BHND Jihadharini msitoe sadaka zenu za kuteketezwa mahali popote mnapopaona; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jihadharini msitoe sadaka zenu za kuteketezwa mahali popote mnapopaona; Neno: Bibilia Takatifu Kuweni waangalifu, msitoe dhabihu zenu za kuteketezwa mahali popote mnapopapenda. Neno: Maandiko Matakatifu Kuweni waangalifu, msitoe dhabihu zenu za kuteketezwa mahali popote mnapopapenda. BIBLIA KISWAHILI Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; |
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA akaiendea njia ya Yeroboamu, na kosa lake ambalo kwa hilo aliwakosesha Israeli.
Ila watu walikuwa wakitoa dhabihu katika mahali pa juu, kwa sababu haikuwapo nyumba iliyojengwa kwa jina la BWANA, hata siku zile.
Lakini mahali pa juu hapakuondolewa katika Israeli; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu siku zake zote.
wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.
bali katika mahali atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote ninayokuamuru.
Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika makabila yenu yote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe uende huko;
pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng'ombe na ya kondoo;
Nao wakawafikia hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakasema nao, wakinena,
Mungu na atuzuie tusimwasi BWANA, na kukengeuka hivi leo na kuacha kumfuata BWANA, hata mkajenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, au sadaka za unga, au dhabihu, mbali na ile madhabahu ya BWANA, Mungu wetu, iliyo huko mbele ya maskani yake.