Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Kumbukumbu la Torati 11:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nami nitakupa nyasi katika mavue yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ataotesha majani mashambani kwa ajili ya ng'ombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ataotesha majani mashambani kwa ajili ya ng'ombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ataotesha majani mashambani kwa ajili ya ng'ombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Nitawapa majani katika malisho yako kwa ajili ya ng’ombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Nitawapa majani kwa ajili ya ng’ombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nami nitakupa nyasi katika mashamba yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Kumbukumbu la Torati 11:15
12 Marejeleo ya Msalaba  

Ahabu akamwambia Obadia, Pita katika nchi, kwenye chemchemi zote za maji, na vijito vyote; labda tutapata majani, tuwahifadhi hai farasi na nyumbu, tusipate hasara ya hao wanyama wote.


Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi,


Naam, kulungu naye uwandani amezaa, Akamwacha mwanawe kwa kuwa hakuna majani.


Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng'ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamehangaika.


BWANA akajibu, akawaambia watu wake; Tazameni, nitawaletea nafaka, na divai, na mafuta, nanyi mtashiba kwa vitu hivyo; wala sitawafanya tena kuwa aibu kati ya mataifa;


Msiogope, enyi wanyama wa porini; maana malisho ya jangwani yanatoa miche, na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu inatoa nguvu zake.


Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.


Tena kupura nafaka kwenu kutaendelea hata wakati wa kuvuna zabibu, na kuvuna zabibu kutaendelea hata wakati wa kupanda mbegu; nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, na kuishi katika nchi yenu salama.


Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamtosheki na vinywaji; mnajivika nguo lakini hampati joto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotobokatoboka.


na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vilivyochimbwa usivyochimba wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba;


Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa.