BWANA akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote;
Kumbukumbu la Torati 11:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC nayo ni nchi itunzwayo na BWANA, Mungu wako; macho ya BWANA Mungu wako, ya juu yake, tangu mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, huitunza; Mwenyezi-Mungu huiangalia daima tangu mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka. Biblia Habari Njema - BHND nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, huitunza; Mwenyezi-Mungu huiangalia daima tangu mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, huitunza; Mwenyezi-Mungu huiangalia daima tangu mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka. Neno: Bibilia Takatifu Ni nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anaitunza; macho ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka. Neno: Maandiko Matakatifu Ni nchi ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu anaitunza; macho ya bwana Mwenyezi Mungu wenu yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka. BIBLIA KISWAHILI nayo ni nchi itunzwayo na BWANA, Mungu wako; macho ya BWANA Mungu wako, yako juu yake, tangu mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka. |
BWANA akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote;
hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya chakula na mashamba ya mizabibu, nchi ya mafuta ya mzeituni na asali, ili mpate kuishi, msife; wala msimsikilize Hezekia, awadanganyapo, akisema, BWANA atatuokoa.
Lakini jicho la Mungu lilikuwa likiwaelekea wazee wa Wayahudi, hao wasiwazuie hadi habari ile imfikie Dario, ndipo jawabu itakapopatikana kwa waraka.
hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu.
Kwa maana nitawaelekezea macho yangu, wapate mema, nami nitawaingiza katika nchi hii tena; nami nitawajenga, wala sitawabomoa; nitawapanda wala sitawang'oa.