Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.
Kumbukumbu la Torati 10:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA akaniambia, Ondoka, uendelee na safari yako ukiwaongoza watu; nao wataingia waimiliki nchi, niliyowaapia baba zao ya kuwa nitawapa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha akaniambia ‘Ondoka uendelee na safari yako ukiwaongoza watu ili waweze kuingia na kuimiliki nchi niliyowaapia babu zenu ya kuwa nitawapa’. Biblia Habari Njema - BHND Kisha akaniambia ‘Ondoka uendelee na safari yako ukiwaongoza watu ili waweze kuingia na kuimiliki nchi niliyowaapia babu zenu ya kuwa nitawapa’. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha akaniambia ‘Ondoka uendelee na safari yako ukiwaongoza watu ili waweze kuingia na kuimiliki nchi niliyowaapia babu zenu ya kuwa nitawapa’. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akaniambia, “Nenda, ukawaongoze watu katika njia yao ili waweze kuingia na kuimiliki nchi ile niliyowaapia baba zao kuwapa.” Neno: Maandiko Matakatifu bwana akaniambia, “Nenda, ukawaongoze watu katika njia yao ili kwamba waweze kuingia na kuimiliki nchi ile niliyowaapia baba zao kuwapa.” BIBLIA KISWAHILI BWANA akaniambia, Ondoka, uendelee na safari yako ukiwaongoza watu; nao wataingia waimiliki nchi, niliyowaapia baba zao ya kuwa nitawapa. |
Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.
BWANA akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii;
Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.
Nikakaa mle mlimani kama hapo kwanza, siku arubaini usiku na mchana; BWANA akanisikiza wakati huo nao; BWANA asitake kukuangamiza.
Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;