Maana tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida, Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?
Kumbukumbu la Torati 1:45 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mkarudi mkalia mbele za BWANA; BWANA asiisikize sauti yenu, wala hakuelekeza masikio yake kwenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndipo mliporudi, mkamlilia Mwenyezi-Mungu, lakini Mwenyezi-Mungu hakuwasikiliza wala hakuwajali. Biblia Habari Njema - BHND Ndipo mliporudi, mkamlilia Mwenyezi-Mungu, lakini Mwenyezi-Mungu hakuwasikiliza wala hakuwajali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndipo mliporudi, mkamlilia Mwenyezi-Mungu, lakini Mwenyezi-Mungu hakuwasikiliza wala hakuwajali. Neno: Bibilia Takatifu Mlirudi na kulia mbele za Mwenyezi Mungu, lakini Mungu hakusikiliza kilio chenu, wala hakuwajali. Neno: Maandiko Matakatifu Mlirudi na kulia mbele za bwana, lakini Mungu hakusikiliza kilio chenu, wala hakuwajali. BIBLIA KISWAHILI Mkarudi mkalia mbele za BWANA; BWANA asiisikize sauti yenu, wala hakuelekeza masikio yake kwenu. |
Maana tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida, Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?
Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
Tunajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.
Maana mnajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.