Elfu moja watakimbia kwa kukemewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima.
Kumbukumbu la Torati 1:42 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA akaniambia, Waambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi siko kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Waambie hao watu wasiende kupigana kwa sababu sipo pamoja nao; wasiende, wasije wakashindwa na adui zao’. Biblia Habari Njema - BHND Naye Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Waambie hao watu wasiende kupigana kwa sababu sipo pamoja nao; wasiende, wasije wakashindwa na adui zao’. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Waambie hao watu wasiende kupigana kwa sababu sipo pamoja nao; wasiende, wasije wakashindwa na adui zao’. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Mwenyezi Mungu aliniambia, “Waambie, ‘Msipande kupigana, kwa sababu sitakuwa pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu.’ ” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini bwana aliniambia, “Waambie, ‘Msipande kupigana, kwa sababu sitakuwa pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu.’ ” BIBLIA KISWAHILI BWANA akaniambia, Waambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi siko kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu. |
Elfu moja watakimbia kwa kukemewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima.
Wajapolea watoto wao, mimi nitawanyang'anya watoto wao, asisalie hata mtu mmoja; naam, ole wao! Nitakapoondoka na kuwaacha.
Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye.
Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu elfu thelathini walioenda vitani kwa miguu.
Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Waisraeli wakapigwa na Wafilisti; waliowaua karibu elfu nne katika uwanja wa vita.