Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa maono, Ukasema, Nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.
Kumbukumbu la Torati 1:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu, na mzigo wenu, na ugomvi wenu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mimi peke yangu nitawezaje kuchukua jukumu hilo zito la kusuluhisha ugomvi wenu? Biblia Habari Njema - BHND Lakini mimi peke yangu nitawezaje kuchukua jukumu hilo zito la kusuluhisha ugomvi wenu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mimi peke yangu nitawezaje kuchukua jukumu hilo zito la kusuluhisha ugomvi wenu? Neno: Bibilia Takatifu Lakini mimi nitawezaje kubeba matatizo yenu, na mizigo yenu, na magomvi yenu peke yangu? Neno: Maandiko Matakatifu Lakini mimi nitawezaje kubeba matatizo yenu, na mizigo yenu, na magomvi yenu peke yangu? BIBLIA KISWAHILI Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu, na mzigo wenu, na ugomvi wenu? |
Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa maono, Ukasema, Nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.
Kwa kweli utajidhoofisha mwenyewe, na hawa watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako.
katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo?
Si kwamba tunatosha sisi wenyewe kufikiri kuwa neno lolote ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu unatoka kwa Mungu.
BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabariki, kama alivyowaahidi.
Jitwalieni watu wenye akili na fahamu, watu wanaojulikana, kwa kadiri ya makabila yenu, nami nitawafanya wawe vichwa juu yenu.