Isaya 7:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tena itakuwa katika siku hiyo kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja, iliyopata fedha elfu moja, patakuwa mahali pa mbigili na miiba tu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huo, kila mahali palipokuwa na mashamba ya mizabibu kwa maelfu ya thamani ya fedha 1,000 kwa kipimo cha hekalu yatakuwa mbigili na miiba mitupu. Biblia Habari Njema - BHND Wakati huo, kila mahali palipokuwa na mashamba ya mizabibu kwa maelfu ya thamani ya fedha 1,000 kwa kipimo cha hekalu yatakuwa mbigili na miiba mitupu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huo, kila mahali palipokuwa na mashamba ya mizabibu kwa maelfu ya thamani ya fedha 1,000 kwa kipimo cha hekalu yatakuwa mbigili na miiba mitupu. Neno: Bibilia Takatifu Katika siku ile, kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja yenye thamani ya shekeli elfu moja za fedha, patakuwa na michongoma na miiba tu. Neno: Maandiko Matakatifu Katika siku ile, kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja yenye thamani ya shekeli 1,000 za fedha, patakuwa na michongoma na miiba tu. BIBLIA KISWAHILI Tena itakuwa katika siku hiyo kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja, iliyopata fedha elfu moja, patakuwa mahali pa mbigili na miiba tu. |
Maana mtataabishwa kwa zaidi kidogo ya mwaka, enyi wanawake mliojikinai; kwa sababu mavuno ya mizabibu yatakoma, wakati wa kuvuna vitu vya mashamba hautakuja.
Kwa maana shamba la mizabibu la eka kumi litatoa bathi moja tu, na homeri ya mbegu itatoa efa tu.
nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
Mtu atakayekwenda huko atakwenda na mishale na upinde; kwa sababu nchi yote itakuwa ina mbigili na miiba.
Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za BWANA, na mbele za hasira yake kali.
Na miji yote yenye watu itakuwa maganjo, nayo nchi itakuwa ukiwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, Hii ndiyo ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa msitu, na wanyama wa mashamba wataila.
Kwa maana, tazama, wamekwenda zao ili kukimbia uharibifu, lakini Misri itawakusanya, Nofu itawazika; vitu vyao vya fedha viwapendezavyo, magugu yatavimiliki; miiba itakuwa katika hema zao.
Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye shamba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia ua, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.
bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.