Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa.
Isaya 7:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Katika siku hiyo itakuwa ya kwamba mtu atalisha ng'ombe jike mchanga na kondoo wawili wa kike; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huo, mtu atafuga ng'ombe mmoja mchanga na kondoo wawili; Biblia Habari Njema - BHND Wakati huo, mtu atafuga ng'ombe mmoja mchanga na kondoo wawili; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huo, mtu atafuga ng'ombe mmoja mchanga na kondoo wawili; Neno: Bibilia Takatifu Katika siku ile, mtu atahifadhi hai mtamba mmoja na kondoo wawili. Neno: Maandiko Matakatifu Katika siku ile, mtu atahifadhi hai ndama mmoja na kondoo wawili. BIBLIA KISWAHILI Katika siku hiyo itakuwa ya kwamba mtu atalisha ng'ombe jike mchanga na kondoo wawili wa kike; |
Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa.
Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa mahali pa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu.
Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake.
Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi.
Na kwako wewe dalili ndiyo hii; mwaka huu mtakula vitu vimeavyo vyenyewe; na mwaka wa pili mtakula mazao ya mbegu za vitu hivyo; na mwaka wa tatu pandeni mbegu, kavuneni; mkapande mizabibu katika mashamba, mkale matunda yake.
Ndipo wana-kondoo watakapojilisha kama walio katika malisho yao wenyewe, na mahali pao walionenepa, palipoachwa ukiwa, wageni watakula.
Na vilima vyote vilivyolimwa kwa jembe, hutafika huko kwa sababu ya kuiogopa mbigili na miiba, lakini hapo patakuwa mahali pa kupeleka ng'ombe, mahali pa kukanyagwa na kondoo.
Lakini Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawaacha baadhi ya maskini wa watu, waliokuwa hawana kitu, katika nchi ya Yuda, akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba wakati uo huo.