Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Isaya 7:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Jitakie ishara ya BWANA, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Mwombe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, akupe ishara; iwe ni kutoka chini kuzimu au juu mbinguni.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Mwombe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, akupe ishara; iwe ni kutoka chini kuzimu au juu mbinguni.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Mwombe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, akupe ishara; iwe ni kutoka chini kuzimu au juu mbinguni.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Mwombe Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ishara, iwe kwenye vina virefu sana, au kwenye vimo virefu sana.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Mwombe bwana Mwenyezi Mungu wako ishara, iwe kwenye vina virefu sana, au kwenye vimo virefu sana.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Jitakie ishara ya BWANA, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Isaya 7:11
18 Marejeleo ya Msalaba  

Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena BWANA, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika.


Na kwako wewe hii ndiyo dalili; mwaka huu mtakula vitu viotavyo vyenyewe; na mwaka wa pili mtakula mazao ya vitu hivyo; na mwaka wa tatu pandeni mbegu, kavuneni; mkapande mashamba ya mizabibu, mkale matunda yake.


Farao atakaponena nanyi, na kuwaambia, Jifanyieni miujiza; ndipo utakapomwambia Haruni, Shika fimbo yako, uibwage chini mbele ya Farao, ili iwe nyoka.


Na kwako wewe dalili ndiyo hii; mwaka huu mtakula vitu vimeavyo vyenyewe; na mwaka wa pili mtakula mazao ya mbegu za vitu hivyo; na mwaka wa tatu pandeni mbegu, kavuneni; mkapande mizabibu katika mashamba, mkale matunda yake.


Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionesha ya kuwa nitapanda niingie nyumbani mwa BWANA?


Badala ya michongoma utamea msonobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.


Tena BWANA akasema na Ahazi akinena,


Lakini Ahazi akasema, Sitaitaka, wala sitamjaribu BWANA.


BWANA akasema hivi, Nenda ukanunue gudulia la mfinyanzi, ukachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa watu, na baadhi ya wazee wa makuhani;


Ndipo hapo utalivunja gudulia lile, mbele ya macho ya watu wale waendao pamoja nawe,


Na hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu, asema BWANA, kwamba mimi nitawaadhibu ninyi mahali hapa, mpate kujua ya kuwa maneno yangu yatasimama juu yenu, kuwaletea mabaya bila shaka;


Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe.