Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.
Isaya 66:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe, halafu niwazuie wasizaliwe? Au mimi mwenye kuwajalia watoto, nitafunga kizazi chao? Mimi Mungu wenu nimesema.” Biblia Habari Njema - BHND Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe, halafu niwazuie wasizaliwe? Au mimi mwenye kuwajalia watoto, nitafunga kizazi chao? Mimi Mungu wenu nimesema.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe, halafu niwazuie wasizaliwe? Au mimi mwenye kuwajalia watoto, nitafunga kizazi chao? Mimi Mungu wenu nimesema.” Neno: Bibilia Takatifu Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa na nisizalishe?” asema Mwenyezi Mungu. “Je, nifunge tumbo la uzazi wakati mimi ndiye nizalishaye?” asema Mungu wako. Neno: Maandiko Matakatifu Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa na nisizalishe?” asema bwana. “Je, nifunge tumbo la uzazi wakati mimi ndiye nizalishaye?” asema Mungu wako. BIBLIA KISWAHILI Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako. |
Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.
Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wako tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.
Uchungu wa mwanamke mwenye mimba utampata; yeye ni mwana asiye na akili; maana wakati umewadia, ambao haimpasi kukawia mahali wapenyapo watoto.