Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.
Isaya 66:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama mama amtulizavyo mwanawe, kadhalika nami nitawatuliza; mtatulizwa mjini Yerusalemu. Biblia Habari Njema - BHND Kama mama amtulizavyo mwanawe, kadhalika nami nitawatuliza; mtatulizwa mjini Yerusalemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama mama amtulizavyo mwanawe, kadhalika nami nitawatuliza; mtatulizwa mjini Yerusalemu. Neno: Bibilia Takatifu Kama mama anavyomfariji mtoto wake, ndivyo nitakavyokufariji wewe, nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.” Neno: Maandiko Matakatifu Kama mama anavyomfariji mtoto wake, ndivyo nitakavyokufariji wewe, nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.” BIBLIA KISWAHILI Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu. |
Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.
Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.
Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.
Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Naye atawahurumia watu wake walioteswa.
Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani?
Maana BWANA ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya nyika yake kuwa kama bustani ya Edeni, na jangwa lake kama bustani ya BWANA; shangwe na furaha zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba.
Furahini pamoja na Yerusalemu, shangilieni kwa ajili yake, ninyi nyote mmpendao; furahini pamoja naye kwa furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake;
Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;
atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.